KUHUSU

Ufafanuzi wa Zana ya Kutathmini Mahitaji (NAT):

Zana ya Kutathmini Mahitaji (NAT) ilitengenezwa kulingana na mbinu za haki za binadamu na hutumiwa chini ya mradi wa AMiD ili kuwatathmini wahamiaji wenye ulemavu. NAT hufuata Kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wenye Ulemavu (UNCRPD) katika juhudi za kuweka mahitaji na mapendeleo ya mtu kama kipaumbele katika mchakato wa kutathmini ulemavu. Kwa sababu hii, maswali ya NAT yameundwa na kutengenezwa kwa njia nzuri na inayoweza kufikiwa ili kutoa nafasi kwa sauti za watu kuweza kusikilizwa. NAT itaruhusu uratibu mwafaka, kushiriki maelezo, tathmini, ulinganisho na uchanganuzi Ulaya nzima.

Kanuni

  1. Haki za Binadamu: NAT inazingatiwa kuwa nyenzo ya kusaidia kuhamasisha kuhusu haki za binadamu. Zana hii haipaswi kutumiwa kama kipimo cha uchunguzi wa kimatibabu lakini kama zana ya haki za binadamu ambayo hufuata kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wenye Ulemavu (UNCRPD) ambapo mahitaji na mapendeleo ya mtu ndio msingi wa fikra kuhusu ulemavu.
  2. Mbinu ya taaluma mbalimbali: NAT imeundwa na kutengenezwa kwa njia inayoweza kufikiwa na rahisi zaidi kama iwezekanavyo. Mbinu hii huhakikisha kwamba wataalamu tofauti wanaweza kuchukua na kutumia NAT katika kazi zao za kila siku. Kwa wale ambao wangependa kupata maelezo zaidi kuhusu maeneo ya “ulemavu” na “uhamiaji” kwa kuwa maeneo hayo ndio yanayoshughulikiwa na kanuni za NAT na kwa ujumla na mradi wa AMiD, tafadhali angalia AMiD training modules.
  3. Ubinadamu: maswali yaliyojumuishwa katika NAT yameandikwa kwa njia wazi. Hii hutoa uwezekano wa mhamiaji kuonyesha mahitaji na matamanio yake bila kuhisi shinikizo la kujibu maswali ya aina ya ‘moja kwa moja’. Hii itamfanya mhamiaji kuhisi vizuri katika mpangilio mzuri zaidi ambao utamwezesha kuelezea hadithi yake ya kibinafsi kwa njia rahisi zaidi.

Je, madhumuni ya Zana ya Kutathmini Mahitaji ni nini?

Idadi ya watu katika Muungano wa Ulaya inaendelea kuwa na watu mbalimbali kama matokeo ya idadi inayokua ya wahamiaji na wakimbizi, ambayo sehemu ndogo muhimu ni ya watu wenye ulemavu. Kulingana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wenye Ulemavu, ‘watu wenye ulemavu ni pamoja na wale walio na matatizo ya muda mrefu ya kimwili, kiakili, au kihisia ambayo yakihusishwa na vikwazo vingine yanaweza kuzuia kushiriki kwao kikamilifu na kwa ufanisi katika jamii kwa kiwango sawa na wengine’ (UNCRPD, 2006, kifungu cha 1, uku. 4).

Mradi wa AMiD utawezesha utaratibu wa njia ya kawaida ya Muungano wa Ulaya katika kuwatathmini wahamiaji wenye ulemavu, kuboresha ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).

Kwa nini zana hii ilitengenezwa?

NAT ni jukwaa ingiliani la kuwatambua wahamiaji wenye ulemavu, wanapowasili katika Muungano wa Ulaya. Malengo ya NAT ni kama yafuatayo:

  • Kuwezesha Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na serikali za mitaa kutathmini na kuwasaidia wahamiaji wenye ulemavu na majibu ya kutosha katika Muungano wa Ulaya.
  • Kuboresha mchakato wao wa usajili, kwa kuwa unaweza kutumiwa wakati wowote wa utaratibu wa kutafuta kimbilio na/au mchakato wa mapokezi.
  • Kuongezea ufahamu na majibu ya wataalamu mbalimbali wanaofanya kazi na wahamiaji na/au watu wenye ulemavu.
  • Kuhakikisha ufikiaji wa huduma mwafaka za usaidizi.

NAT imeundwa ili kuunga mkono Muuungano wa Ulaya [EU] na Nchi Wanachama wa EU katika kutekeleza majukumu yao chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wenye Ulemavu, Mwelekezo wa Hali za Mapokezi (2013/33EU) na Mwelekezo wa Taratibu za Kutafuta Kimbilio (2013/32/EU):

  • Utambuaji lazima ufanywe ndani ya muda unaofaa baada ya maombi ya ulinzi wa kimataifa kufanywa, na unapaswa kuendelea (Kifungu cha 22 RCD kilichofanyizwa upya na Kifungu cha 24 APD kilichofanyizwa upya).
  • Nchi Wanachama wana jukumu la kuzingatia hali mahususi za waombaji wanaohitaji msaada maalum wa mapokezi (Kifungu cha 21 RCD kilichofanyizwa upya) na hakikisho maalum za utaratibu (Orodha ya 29 APD iliyofanyizwa upya). Zana hii inaweza kujumuishwa na Nchi Wanachama katika mpangilio wa mbinu kamili zaidi ya utambulisho. Mbinu ya matumizi yake itategemea mpangilio na mahitaji ya kitaifa. (Imetolewa kwa: zana ya IPSN).

Ni nani anayepaswa kutumia zana hii?

Mfanyakazi anayewajibika
Neno ‘mfanyakazi anayewajibika’ linatumiwa kwa njia ya ujumla ili kujumuisha watu wote ambao wanaweza kushiriki na kuingiliana na mwombaji wakati wa utaratibu wa mahojiano ya ulinzi wa kimataifa. Kwa mfano, neno hilo linaweza kujumuisha maafisa, maafisa wa mapokezi, wahudumu wa jamii, maafisa wa kesi wa mamlaka yanayotoa maamuzi, wafanyakazi katika mstari wa mbele wanaofanya kazi moja kwa moja na wahamiaji, mameneja/wasimamizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), watumishi wa umma, watu wa kujitolea, n.k. Hakuna haja ya ufahamu wa kitaalamu katika nyanja za dawa, saikolojia na nyanja nyingine husika ili kutumia zana hii. Zana hii imeundwa hasa ili kuwatambua watu wenye ulemavu, na kwa hivyo utambulisho huo unaweza kuwa tu wa kwanza na huenda ukahitaji kuelekezwa kwa mtaalamu ili kufuatilia. Zaidi ya hayo, zana hii hupewa mfanyakazi mmoja anayewajibika na kwa hivyo mbinu ya utaalamu mbalimbali ya utambuaji na usaidizi, inayohusisha wataalamu wengine kutoka nyanja tofauti, inapendekezwa sana na inaweza kukuzwa kama zoezi zuri. Inaweza pia kuwa msaada kwa daktari mwingine yeyote anayewasiliana na waombaji wa ulinzi wa kimataifa. Mfanyakazi hawezi kuchukuliwa kuwa anawajibika kwa maelezo yoyote ya kupotosha au yasiyo ya kweli yanayotolewa na mhojiwa.

Jinsi ya kutumia sehemu tofauti za zana?

Msingi wetu wa kuunda zana hii ni kushughulikia mchakato wa utambuaji na usaidizi kwa njia ya jumla na ya ubinadamu zaidi kwa waombaji. Kuna njia nyingi tofauti za kutumia NAT, kulingana na kisa husika, aina ya maelezo uliyo nayo tayari, na lengo la utambulisho. Lengo la NAT ni kukusanya maelezo kuhusu idadi ya waombaji ambao hupitia mchakato wa utambulisho na kuwaunga mkono kupitia huduma zinazopatikana. Kwa hivyo, kutumia viashirio kwa kawaida kunaweza kuchukuliwa kama 'hatua ya kwanza'. Kwanza, tafadhali chukua nafasi hii kujifahamisha zana hii. Wakati wa hatua hii, kama afisa anayewajibika, unahimizwa kuunda mazingira mazuri ya mahojiano, kwa kuwasiliana na mwombaji kwa njia isiyo rasmi sana. Kwa mfano, unaweza kumuuliza kuhusu hadithi yake ya kibinafsi (Swali la 1) ili kumpa nafasi ya kujielezea waziwazi. Isitoshe, ni muhimu kukumbuka kwamba si muhimu kufuata maswali yote yaliyotolewa. Kwa mfano, ikiwa unahisi umekusanya maelezo muhimu kuhusu hadithi ya kibinafsi ya mwombaji au mwombaji hayuko tayari kutoa maelezo ya ziada basi unaweza kuruka swali moja na uendelee na lifuatalo kwa kubofya kitufe cha “Inayofuata”.

Kisha itakulazimu ufanye tathmini kulingana na maelezo uliyoyakusanya kuhusu kisa hicho, maelezo mengine ambayo tayari unayo na ufahamu na uzoefu wako wa sasa kwa kupitia kila moja ya kiashiriaji na kuunda ripoti ya mwisho ('hatua ya 2'). Kulingana na jukumu lako katika mfumo wa kutafuta kimbilio, unaweza kupendekeza shirika linalofaa kutoka kwenye orodha iliyotolewa katika zana kwa msaada unaomfaa zaidi mwombaji ('hatua ya 3').

Tafadhali hakikisha kwamba umemhoji mwombaji kabla ya mwisho wa mahojiano kama sehemu ya mchakato wote ('hatua ya 4').

Utambuaji na utathmini unafaa kuwa kwa misingi ya mtu binafsi. Zana hii imetengenezwa ili kuwatambua watu wenye ulemavu na kutoa msaada unaofaa wakati wa mchakato wa utambulisho. Kwa hivyo, lengo lake si kuwapanga waombaji kulingana na kategoria fulani au kutoa jibu la jumla kwa mahitaji yanayoweza kutokea, lakini kutoa mwongozo ili kumwongoza mtumiaji katika mchakato ambao unapaswa kuhakikisha kwamba mahitaji ya kibinafsi ya mwombaji fulani yameshughulikiwa, na kupendekezewa shirika linalofaa la kumsaidia. Kulingana na mahitaji yako kama mtumiaji na kama utambulisho umefanyika tayari, unaweza kutumia maswali (viashiriaji) au kufikia moja kwa moja kategoria inayofaa na awamu fulani ya msaada ambayo unataka.

Ripoti inayoweza kuchapishwa: Mara tu unapohisi kwamba umekusanya maelezo yote unayoyahitaji, unaweza kuhifadhi au kuchapisha ripoti ambayo inatoa muhtasari wa maelezo ya utambulisho na inayoangazia hatua za kuchukua.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu bofya hapa.

Amif EU disclaimer

This website was funded by the European Union’s Asylum, Migration and Integration Fund. The content represents the views of the author only and is his/her sole responsibility. The European Commission does not accept any responsibility for use that may be made of the information it contains. Project Number: [AMIF-2016-AG-INT-776055] Privacy Policy

Copyright © 2018 - AMiD Project